Mkuu wa jeshi la Sudan atangaza kuunda Baraza la mpito la Utawala
2021-11-12 09:20:23| CRI

Mkuu wa jeshi la Sudan atangaza kuunda Baraza la mpito la Utawala_fororder_无标题

Kamanda mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Sudan, Jenerali Abdel Fattah Al-Burhan ametoa tangazo la kikatiba, akiunda Baraza la Mpito la Utawala atakaloliongoza mwenyewe.

Tangazo hilo linamtaja Jenerali Al-Burhan kuwa Mwenyekiti wa Baraza hilo, na makamu mwenyekiti ni Jenerali Mohamed Hamdan Daqlu, pamoja na wajumbe 11 wa Baraza hilo.

Wakati huohuo, Shirikiso la Wanataaluma la Sudan, ambalo ni moja kati ya makundi yanayoongoza maandamano nchini humo, limetangaza kupinga uteuzi wa Baraza hilo, likisema kamanda wa jeshi hana haki ya kuchukua hatua hiyo.