Marais wa China na Marekani kufanya mazungumzo kwa njia ya mtandao
2021-11-13 15:33:47| CRI

Marais wa China na Marekani kufanya mazungumzo kwa njia ya mtandao_fororder_src=http___news.xhby.net_zt_zzccfkyq_yw_202003_W020200331629307219780.jpeg&refer=http___news.xhby

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Hua Chunying ametangaza kuwa, rais Xi Jinping wa China atafanya mazungumzo na mwenzake wa Marekani Joe Biden kwa njia ya mtandao tarehe 16 asubuhi, ili kubadilishana maoni kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili na masuala yanayojaliwa nao kwa pamoja.