Nigeria yaikemea vikali NGO ya Marekani kwa kuisingizia serikali yake kudhamini ugaidi
2021-11-15 09:10:23| CRI

Serikali ya Nigeria imeelezea madai ya Shirika lisilo la faida la Marekani kwamba serikali inadhamini ugaidi kuwa ni “usumbufu unaochukiza” uliopangwa na wale wanaotaka kudhoofisha mapambano yanayoendelea dhidi ya ugaidi na ujambazi nchini humo.

Kwenye taarifa iliyotolewa Jumapili, Waziri wa Habari na Utamaduni Lai Mohammed amesema huo wanaouita utetezi Duniani wa Kutokomeza Ugaidi (GATE) ni kero kubwa ambayo inapaswa kupuuzwa, hasa kwasababu inachanganya. 

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari, Ijumaa GATE iliiomba ofisi ya waziri wa mambo ya nje ya Marekani, ikiitaka serikali ya nchi hiyo kuwataja maafisa kadhaa wa serikali ya Nigeria kama wadhamini wa ugaidi, na kudai kwamba “viashiria vyote vinaonesha kuwa kinachotokea Nigeria ni udhamini wa ugaidi unaofanywa na taifa”.