Rais Xi atuma barua ya pongezi kwenye kongamano la sita la watu wa China na Afrika
2021-11-15 19:04:09| cri

Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwenye kongamano la sita la watu wa China na Afrika ambalo lilifunguliwa jana Jumatatu mjini Beijing.

Kwenye barua yake rais Xi amesema dunia ipo kwenye zama za maendeleo na mabadiliko makubwa, ambapo China na Afrika zinakabiliwa na fursa na changamoto mpya, na zinahitajika kushikilia na kuendeleza amani, maendeleo, usawa, haki, demokrasia na uhuru, mambo ambayo ni thamani ya pamoja ya binadamu.

Amesisitiza kuwa pande mbili zinapaswa kuimarisha mshikamano na ushirikiano, kuhimiza ustawi na maendeleo, na kushirikiana pamoja kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja ya binadamu. Aidha ametaka jukwaa hilo kuimarisha jukumu lake kama daraja la kusaidia kuimarisha ushirikiano wa kina wa kimkakati wa China na Afrika, kuhimiza maelewano baina ya watu, na kutimiza dhana ya jumuiya China na Afrika yenye hatma ya pamoja.