Marais wa China na Marekani waongea kwa njia ya video
2021-11-16 09:41:58| CRI

Marais wa China na Marekani waongea kwa njia ya video_fororder_头图中美

Rais wa China Xi Jinping leo asubuhi amefanya mazungumzo kwa njia ya video na mwenzake wa Marekani Joe Biden ambapo wamebadilishana maoni kuhusu uhusiano baina ya China na Marekani juu ya masuala wanayoyafuatilia kwa pamoja.

Kwenye mazungumzo yao rais Xi amebainisha kuwa hivi sasa, China na Marekani zipo kwenye hatua muhimu kabisa ya maendeleo, na jamii ya binadamu duniani pia inakabiliwa na changamoto nyingi. Zikiwa nchi zenye uchumi mkubwa duniani na wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, China na Marekani zinapaswa kuimarisha mawasiliano na ushirikiano wao, sio tu kwenye kushughulikia masuala husika ya ndani, bali pia kubeba majukumu yanayostahili ya kimataifa.