Kongamano la maendeleo ya Xinjiang la China 2021 lafanyika jijini Beijing
2021-11-16 13:42:09| Kongamano la maendeleo ya Xinjiang la China 2021 lafanyika jijini Beijing

Kongamano la maendeleo ya Xinjiang la China 2021 limefanyika jijini Beijing. Wajumbe kutoka nchi na mashirika zaidi ya 30 duniani wamehudhuria kongamano hilo. Washiriki wa kongamano hilo wamepongaza mafanikio yaliyopatikana katika shughuli mbalimbali mkoani Xinjiang tangu mkutano mkuu wa 18 wa Chama cha Kikomunisiti cha China, huku wakitoa mapendekezo mbalimbali kuhusu kuhimiza maendeleo yenye sifa ya juu ya Xinjiang na “Ukanda Mmoja na Njia Moja”.

Kaulimbiu ya kongamano hilo ni “Ujenzi wa pamoja wa ‘Ukanda Mmoja na Njia Moja’na maendeleo ya Xinjiang”. Mwaka 2015, serikali ya China ilitangaza na kuhimiza ujenzi wa pamoja wa “Ukanda Mmoja na Njia Moja” na kuweka bayana kuijengea Xinjiang kuwa kiini cha eneo la kiuchumi la Njia ya Hariri. Sasa Xinjiang imekuwa njia muhimu ya mawasiliano kati ya nchi za “Ukanda Mmoja na Njia Moja”, huku ikitimiza maendeleo ya kasi, utulivu wa kijamii na uboreshaji wa maisha.