China yaitaka Marekani ishughulikie suala la Taiwan kwa busara na kwa usahihi
2021-11-16 09:39:11| CRI

China yaitaka Marekani ishughulikie suala la Taiwan kwa busara na kwa usahihi_fororder_台湾

China imeitaka Marekani ishughulikie suala la Taiwan kwa usahihi na njia ya busara, ili kuepuka kuharibu uhusiano kati ya nchi hizo mbili pamoja na amani na utulivu wa Mlango Bahari wa Taiwan.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian jana alisema hayo wakati akijibu swali juu ya kauli za hivi karibuni za waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Antony Blinken, ambaye alisema Marekani inadhamiria kukahikikisha kuwa Taiwan ina uwezo wa kujilinda chini ya ile inayoitwa “Sheria ya uhusiano na Taiwan”.

Zhao alisema China inapinga kithabiti kauli na vitendo vya Marekani visivyo sahihi, na kuitaka Marekani ishikilie kanuni ya kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja za China na Marekani. Ameongeza kuwa zile zinazoitwa “Sheria ya uhusiano na Taiwan” na “Ahadi Sita” zote zilitengenezwa na baadhi ya makundi ya kisiasa nchini Marekani, na zimeiweka sheria ya ndani ya Marekani juu ya majukumu ya kimataifa, jambo ambalo ni haramu na batili.