Waziri mkuu wa China ataka kuwepo kwa ushirikiano wa karibu kati ya serikali za mikoa za China na Afrika
2021-11-17 10:29:08| CRI

Waziri mkuu wa China ataka kuwepo kwa ushirikiano wa karibu kati ya serikali za mikoa za China na Afrika_fororder_11

Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang ametoa wito kwa China na Afrika kuongeza ushirikiano wa kivitendo ili kujenga siku nzuri za baadaye kwa ajili ya watu bilioni 2.7 wa pande hizo mbili.

Li alisema hayo jana akihutubia kwa njia ya video kwenye Kongamano la Nne kuhusu Ushirikiano wa Serikali za Mikoa za China na Afrika. Akielezea urafiki kati ya China na Afrika kuwa imara, Bw. Li amesema China inapenda kuongeza msaada wa chanjo na vifaa vya kupambana na janga la COVID-19 katika nchi za Afrika kwa mujibu wa mahitaji yake ili kulinda vizuri afya za watu wa Afrika.

Bw. Li ameongeza kuwa China inapenda kuunganisha mikakati yake ya maendeleo na ya Afrika, kubadilishana maarifa kuhusu usimamizi wa miji, kupunguza umaskini, kujenga jamii na kilimo cha kisasa na kuhimiza ushirikiano kati ya miji rafiki.