Mkutano wa 8 wa mawaziri wa FOCAC kuangazia ushirikiano katika sekta mpya
2021-11-18 09:29:31| CRI

Mkutano wa 8 wa mawaziri wa FOCAC kuangazia ushirikiano katika sekta mpya_fororder_中非合作论坛

Naibu waziri wa biashara wa China Bw. Qian Keming amesema mkutano wa 8 wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utaofanyika mwishoni mwa mwezi huu mjini Dakar, Senegal utaangazia fursa mpya za ushirikiano haswa katika sekta mpya ikiwemo afya, uchumi wa kidigitali na maendeleo ya kijani.

Bw. Qian ameeleza kuwa ukiwa na kauli mbiu ya “kuimarisha ushirikiano wa kiwenzi wa China na Afrika, kuhimiza maendeleo endelevu na kujenga jumuiya yenye hatma ya pamoja kati ya China na Afrika katika zama mpya”, mkutano huo utatangaza hatua mpya za ushirikiano ambazo hazitajikita kwenye sekta za jadi tu, bali pia za kusaidia Afrika kufufua maendeleo, kupunguza umaskini, kukuza biashara na uwekezaji, pamoja na kupanua ushirikiano katika sekta mpya.

Imefahamika kuwa “dira ya mwaka 2035 ya ushirikiano kati ya China na Afrika” itatangazwa katika mkutano huo, waraka ambao Bw. Qian amesema utakuwa msingi wa ushirikiano kati ya China na Afrika katika miaka 15 ijayo, na kufanya hatua mpya zinazotangazwa na mkutano wa FOCAC ziwe za kuangalia mbali, za kimfumo na endelevu.