China kutenga tena mkopo maalumu kwa ajili ya matumizi salama na yenye ufanisi ya makaa ya mawe
2021-11-18 09:22:58| CRI

Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang jana aliendesha mkutano wa Baraza la serikali ya China, ambao umeamua kuwa China itatenga tena mkopo maalumu kwa ajili ya matumizi salama na yenye ufanisi ya makaa ya mawe, ili kuhimiza ukuaji usiosababisha uchafuzi na wenye kiwango cha chini cha kaboni.

Makaa ya mawe ni maliasili kuu ya nishati nchini China, na ni lazima kuongeza kiwango cha matumizi salama na yenye ufanisi ya makaa ya mawe yanayoendana na hali halisi ya China. Li amesema kwa hivi sasa makaa ya mawe ni chanzo cha nishati ambacho tunaweza kujitegemea kwenye usambazaji, hali ambayo inahusiana na maendeleo ya China, na inahitaji kufanya mabadiliko kwenye njia ya maendeleo.

Ameongeza kuwa chini ya msingi wa fedha zilizotolewa hapo awali kwa ajili ya kusaidia kupunguza utoaji wa hewa ya ukaa, China itatenga tena mkopo maalumu wenye thamani ya yuan bilioni 200 (sawa na dola takriban bilioni 31.3 za kimarekani) kwa ajili ya matumizi salama na yenye ufanisi ya makaa ya mawe.