Msomi wa Kenya asema michezo ya Olimpiki ya Beijing ya majira ya baridi itahimiza mshikamano, amani na mageuzi ya kijani duniani
2021-11-18 09:26:21| CRI

Msomi wa Kenya amesema michezo ya Olimpiki ya Beijing ya majira ya baridi ya mwaka 2022, itatoa fursa ya kuinua majukumu ya China katika kuhimiza mshikamano, amani na mageuzi ya kijani duniani.

Cavince Adhere, msomi wa masuala ya uhusiano wa kimataifa anayeshughulikia uhusiano kati ya China na Afrika amesema michezo hii mikubwa, ambayo maandalizi yake yamefanyika kwa kasi pia itaonesha nguvu laini za China, kielelezo cha ustaarabu wa ikolojia na utendaji wake mzuri katika vita dhidi ya COVID-19. Wakati akifafanua kuwa michezo ya Olimpiki imehimiza umoja na werevu, Adhere amesema makala ya 2022 ya Beijing yatainua kiwango cha wema wa pamoja wa binadamu.

Pia ameipongeza China kwa maandalizi yake mazuri na kuongeza kuwa kuandaa michezo ya Olimpiki katika kipindi ambacho tunakabiliwa na janga la COVID-19 kwa miaka miwili iliyopita ni kazi kubwa.