Waziri Mkuu wa China aahidi kwamba China itapanua zaidi ufunguaji mlango
2021-11-18 09:25:05| CRI

Waziri Mkuu wa China aahidi kwamba China itapanua zaidi ufunguaji mlango_fororder_李克强世界经济论坛

China itapanua zaidi ufunguaji wake mlango bila kuyumba na kujenga mazingira ya biashara yenye mwelekeo wa soko, msingi wa sheria na kufikia viwango vya kimataifa.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa China Li Keqiang wakati alipohudhuria mazungumzo maalumu kwa njia ya mtandao wa internet na viongozi wa biashara duniani ulioandaliwa na Jukwaa la Uchumi Duniani juzi Jumanne, ambapo karibu wajasiriamali 400 kutoka nchi 40 duniani walihudhuria mkutano huo.

Bw. Li amebainisha kuwa uchumi wa China umefungamana na uchumi wa dunia, na kufungua mlango ndio sera ya msingi ya taifa ya China. Ameahidi kwamba China itaendelea kufungua mlango wake, kukuza ushirikiano katika nyanja mbalimbali na ngazi mbalimbali za kimataifa, kuhudumia vyombo mbalimbali vya soko kwa usawa, na kulinda haki miliki ya ubunifu kwa mujibu wa sheria. Aidha Bw. Li amesema China ni soko kubwa duniani, na ni sehemu muhimu ya uwekezaji, hivyo inakaribisha makampuni kutoka maeneo mbalimbali duniani kuwekeza na kufanya biashara yao.