Uchokozi unaofanywa na Lithuania kuhusu suala la Taiwan utashindwa
2021-11-19 20:16:13| cri

Lithuania imeonyesha undani wake halisi baada ya kuichokoza China waziwazi kuhusu swala la Taiwan. Na mamlaka ya Taiwan inayounga mkono kujitenga na China itafanya makosa kama  itafuata hatua ya Lithuania wakati kisiwa hicho kinajaribu kuingia zaidi kwenye jukwaa la kimataifa. 

Wizara ya Mambo ya Nje ya China usiku wa kuamkia leo imepinga vikali Lithuania kuidhinisha kuanzishwa kwa kile kinachoitwa Ofisi ya Mwakilishi wa Taiwan nchini Lithuania, ili kuonyesha kuwa kamwe China haitakubali kurudi nyumba kuhusu sera ya China moja. .

Ukweli haupingiki kuwa kuna China moja tu duniani, na Taiwan ni sehemu isiyoweza kutengwa ya ardhi ya China, na serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ndiyo serikali pekee kisheria inayoiwakilisha China nzima.

Upande wa Lithuania utawajibika kwa matokeo yote yanayofuata kwa sababu ya hila yake ya kuanzisha uhusiano rasmi na kisiwa hicho. Kwa hakika, imekiuka ahadi yake iliyotoa ilipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Jamhuri ya watu wa China mwaka 1991, na kuilingilia mstari mwekundu wa China.

Inaonekana kwamba Lithuania inakabiliwa na uchaguzi kati ya China na nguvu inaoipinga China, ambayo sasa inaamini kuwa kadi ya Taiwan inaweza kuwa karata ya kuvuruga juhudi za kuiunganisha China na kuzuia maendeleo yake. Sasa imetoa jibu wazi zaidi kwa kujiweka kama kibaraka anayetumiwa na kambi ya kisiasa inayoipinga China.