Chama cha CPC chaanza mchakato wa uchaguzi wa wajumbe wake wa Mkutano mkuu wa 20
2021-11-19 10:42:51| CRI

Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) imetoa tangazo la uchaguzi wa wajumbe wa Mkutano mkuu wa 20 wa CPC, na kuweka kikamilifu mipango ya kazi hiyo.

Taarifa rasmi iliyotolewa jana imesema Idara ya Mipango ya Kamati kuu ya CPC imeweka mpango wa kina kuhusu uchaguzi huo. Wajumbe 2,300 watachaguliwa kwenye maeneo 38 ya uchaguzi kote nchini.

Mkutano wa 6 wa wajumbe wote wa kamati kuu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China uliomalizika mapema mwezi huu umeamua kuwa, CPC kitafanya Mkutano wake mkuu wa 20 katika nusu ya pili ya mwaka 2022 mjini Beijing, na utakuwa ni mkutano muhimu kwa China wakati ambao inaanza safari mpya ya kuijenga China kuwa nchi ya ujamaa ya kisasa kwa pande zote na kujitihidi kutimiza lengo la miaka mia moja mingine ya pili, ambalo ni tukio kubwa katika shughuli za kisiasa za CPC na China.