China yapinga vikali Lithuania kuridhia kuanzishwa kwa eti “ofisi ya mwalikishi ya Taiwan nchini Lithuania”
2021-11-19 10:47:12| CRI

China yapinga vikali Lithuania kuridhia kuanzishwa kwa eti “ofisi ya mwalikishi ya Taiwan nchini Lithuania”_fororder_立陶宛

China imepinga vikali serikali ya Lithuania kwa kuridhia kuanzishwa kwa eti “Ofisi ya Mwakilishi ya Taiwan nchini Lithuania”.

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema kitendo hiki kimetengeneza kwa makosa “China moja, Taiwan moja” duniani, kukiuka wazi kanuni ya kuwepo kwa China moja, na kwenda kinyume na ahadi ya kisiasa iliyotoa Lithuania ilipojenga uhusiano wa kibalozi na Jamhuri ya Watu wa China, kuharibu mamlaka na ukamilifu wa ardhi ya China na kuingilia kati mambo ya ndani ya China.

China imesema itachukua hatua zote kulinda mamlaka ya taifa na ukamilifu wa ardhi, na Lithuania itawajibika na matokeo yote mabaya.