China na Russia zapinga kuweka muundo mmoja wa demokrasia kwa nchi zote
2021-11-20 13:37:19| Cri

 

Ujumbe wa Kudumu wa China na Russia kwenye ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Geneva umefanya semina kwa njia ya video iitwayo“Demokrasia na Haki za Binadamu: Malengo ya Pamoja, Njia Mbalimbaliofauti”, ambayo ilihudhuhuriwa na watu 130 wakiwemo wawakilishi wa kudumu na wanadiplomasia waandamizi kutoka nchi zipatazo 60.

Kaimu kiongozi wa ujumbe wa kudumu wa China mjini Geneva Li Song amesema demokrasia ni lengo la pamoja la binadamu wote, na haki za binadamu ni ndoto na matakwa ya pamoja ya watu wa nchi mbalimbali. Nchi moja ina demokrasia au hapana, ni wananchi wake wana sauti ya kuamua. Amesisitiza kuwa demokrasia na haki za binadamu sio visingizio vya kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi, kitendo ambacho kinaweza kuzusha mgongano na hata ghasia na maafa.

Naye mwakilishi wa kudumu wa Russia mjini Geneva Gennady Gatilo alisema sifa za tamaduni tofauti, vigezo vya maadili na thamani vinatakiwa kuzingatiwa katika kutafuta demokrasia na haki za binadamu, na haikubaliki kwa baadhi za nchi zinazojitangazia kama ni “ngome ya demokrasia”kushikilia fikra ya vita ya baridi na kuamua“vipimo vya demokrasia”.