China yaamua kushusha kiwango cha uhusiano wake na Lithuania
2021-11-21 15:49:33| Cri

Novemba 18 Lithuania iliidhinisha mamlaka ya Taiwan kuanzisha “Ofisi ya Mwakilishi wa Taiwan nchini Lithuania” bila ya kujali upinzani wa China, Wizara ya Mambo ya Nje ya China imetoa taarifa ikisema, hatua hii imekwenda kinyume na ahadi ya siasa iliyotoa Lithuania katika taarifa ya kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya pande hizo mbili, kuharibu mamlaka na ukamilifu wa ardhi wa China, na kuingilia kwa nguvu mambo ya ndani ya China. China inaipinga vikali hatua hii ya Lithuania na kuamua kushusha kiwango cha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili hadi kiwango cha charge d'affaires.