Kenya kuanza kutoa huduma kwa watu waliopata chanjo kamili
2021-11-22 09:21:22| cri

Kenya kuanza kutoa huduma kwa watu waliopata chanjo kamili_fororder_肯尼亚非洲

Kenya itawataka watu wanaohitaji huduma za serikali zinazotolewa uso kwa uso kuchanjwa kikamilifu dhidi ya COVID-19 kuanzia Disemba 21.

Waziri wa afya wa Kenya Bw. Mutahi Kagwe amewaambia wanahabari kuwa hatua kali zinatolewa baada ya kuangalia hali ya COVID-19 nchini humo na kuona kuna haja ya kuhakikisha nchi hiyo inakuwa katika njia ya kudhibiti ugonjwa huo. Amesema mashirika yote yanayotoa huduma kwa watu 50 na zaidi yatatakiwa kuweka vibao vinavyohitaji uthibitisho wa chanjo kabla ya kuingia kwenye jengo na wateja wao kuchanjwa kikamilifu.

Kenya pia imetoa agizo la kuwataka wafanyabiashara wote wa magari wapate chanjo kamili na wawe na uthibitisho wa chanjo wakati wote kuanzia Disemba, 21.

Bw. Kagwe amesema watu binafsi pia watahitajika kuonyesha uthibitisho wa chanjo dhidi ya COVID-19 ili waweze kuandikishwa katika mbuga za taifa, hoteli na mikahawa kuanzia siku hiyo.