Rais wa China aendesha mkutano wa kuadhimisha miaka 30 tangu China na ASEAN zianzishe mazungumzo
2021-11-22 15:56:23| CRI

Rais Xi Jinping wa China leo asubuhi kwa njia ya mtandao amehudhuria na kuendesha mkutano wa kilele wa kuadhimisha miaka 30 tangu China na Umoja wa Nchi za Kusini Mashariki mwa Asia (ASEAN) zianzishe utaratibu wa mazungumzo.

Kwenye mkutano huo rais Xi amesisitiza kuwa China daima itaendelea kuwa jirani mwema, rafiki mkubwa na mwenzi mzuri wa ASEAN, na itashikilia kutoa kipaumbele kwa Umoja huo katika mambo yake ya kidiplomasia. Amesema China pia inaunga mkono mshikamano na ujenzi wa Umoja huo, kuunga mkono hadhi kuu ya kikanda ya Umoja huo, na kuunga mkono Umoja huo kufanya kazi kubwa zaidi katika mambo ya kikanda na kimataifa.