Katibu mkuu wa UM atoa wito wa kuzingatia usalama barabarani
2021-11-22 09:25:17| cri

Katibu mkuu wa UM atoa wito wa kuzingatia usalama barabarani_fororder_车祸国际

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito kwa watu kuzingatia usalama barabarani ambapo kila sekunde 24 kuna kifo kimoja kilichosababishwa na ajali za barabarani duniani. Bw Guterres ametoa wito huo katika Siku ya Kimataifa ya Kukumbuka Wahanga wa Ajali za Barabarani ambayo kauli mbiu yake ya mwaka huu ni kusisitiza umuhimu wa kupunguza mwendo kasi barabarani ili kuepusha vifo na majeruhi.

Ametoa wito kwa mataifa, kampuni na watu binafsi kuunga mkono na juhudi za ndani na za dunia kufanya barabara ziwe salama, haswa katika nchi za kipato cha chini na cha kati ambako zaidi ya asilimia 90 ya vifo vinavyosababishwa na ajali za barabarani vinatokea. Pia amezitaka nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuhimiza wahisani kuongeza michango inayohitajika sana ya kifedha na kiufundi kupitia Mfuko wa Usalama Barabarani wa Umoja wa Mataifa.