Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema atakuwa mstari wa mbele kupambana na waasi
2021-11-23 08:30:48| CRI

Waziri Mkuu wa Ethiopia amesema atakuwa mstari wa mbele kupambana na waasi_fororder_埃塞

Waziri Mkuu wa Ethiopia Bw. Abiy Ahmed ametangaza kuwa atakwenda mstari wa mbele kuongoza mapambano dhidi ya waasi kufuatia mgogoro unaozidi kupanuka katika eneo la mashariki mwa nchi hiyo.

Bw. Ahmed ametoa wito kwa “waethiopia wote wazalendo” kuungana naye kwenye mstari wa mbele kupambana na watu wanaoliunga mkono kundi la TPLF. Amesema wakati huu unamhitaji kuliongoza taifa kupita katika kipindi kigumu, na kuanzia leo na kuendelea atakuwa kwenye medani ya vita kuviongoza vikosi vya ulinzi.

Katika miezi miwili iliyopita, mgogoro ulioanza tarehe 4 Novemba mwaka jana katika jimbo la Tigray kati ya majeshi ya serikali na yale yanayolitii kundi la TPLF, umeenea hadi kwenye majimbo ya jirani ya Amhara na Afar.

Mapema mwezi huu Bunge la Ethiopia lilipitisha hali ya dharura ili kupambana na waasi wanaosonga mbele.