Rais wa China atoa barua ya pongezi kwa Mkutano wa Nne wa Kilele wa Vyombo vya Habari Duniani
2021-11-23 09:11:04| cri

Rais Xi Jinping wa China ametoa barua ya pongezi kwa Mkutano wa Nne wa Kilele wa Vyombo vya Habari Duniani uliofanyika mjini Beijing, China.

Rais Xi amesisitiza kuwa sasa mabadiliko makubwa ambayo hayakuwahi kushuhudiwa katika miaka 100 iliyopita yamekutana na janga la virusi vya Corona duniani, ambapo kuathiriana kwao kumeleta hali yenye utatanishi kwa muundo wa kimataifa.

Amesema vyombo vya habari vinabeba majukumu muhimu ya kuhimiza jamii kuitikia masuala yanayoikabili dunia na kukusanya maoni ya pamoja. Rais Xi anatarajia washiriki wa mkutano huo watahimiza maelewano kati yao wakijadili masuala husika na kutoa mchango katika kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

Mkutano wa Nne wa Kilele wa Vyombo vya Habari Duniani uliofanyika jana mjini Beijing umeandaliwa na Shirika la habari la China Xinhua ukiwa na kauli mbiu ya “ Mikakati ya Maendeleo ya Vyombo vya Habari chini ya Athari za COVID-19”.