CMG yatoa filamu ya kumbukumbu ya Vyakula vya Macao kuadhimisha miaka 22 tangu kurudi kwa Macao
2021-11-24 23:00:02| cri

CMG yatoa filamu ya kumbukumbu ya Vyakula vya Macao kuadhimisha miaka 22 tangu kurudi kwa Macao_fororder_微信图片_20211124222839

Ili kuadhimisha miaka 22 tangu Macao kurudi kwa China, filamu ya kumbukumbu ya Vyakula vya Macao iliyotengenezwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) kwa kushirikiana na serikali ya mkoa wa utawala maalumu wa Macao imezinduliwa mjini Guangzhou.

Mkuu wa CMG Shen Haixiong alipohutubia hafla ya uzinduzi wa filamu hiyo, amesema filamu hiyo inaonesha historia na utamaduni vya Macao kupitia vyakula, na utoaji wa filamu hiyo ni matokeo muhimu ya CMG kupanua ushirikiano na serikali ya Macao.

Mkuu wa mkoa wa Macao He Yicheng amesema CMG ni chombo cha habari cha hali ya juu zaidi, na anatarajia kupitia shirika hilo, mambo, hadithi na utamaduni vya Macao vitajulikana zaidi duniani.

He na Shen pia wameshuhudia hafla ya kusaini makubaliano ya kuidhinisha Shirika la Utangazaji la Macao kutangaza vipindi vya michezo vya CMG ikiwemo Michezo ya Olimpiki ya Siku za Baridi ya Beijing, na Michezo ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Duniani itakayofanyika mjini Chengdu.