Kiasi cha mizigo iliyosafirishwa kwa reli ya SGR ya Kenya chaongezeka kwa asilimia 24 katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka
2021-11-24 08:38:04| cri

Kiasi cha mizigo iliyosafirishwa kwa reli ya SGR ya Kenya chaongezeka kwa asilimia 24 katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka_fororder_SGR

Ripoti iliyotolewa Jumanne wiki hii na Shirika la Reli Kenya inaonesha kuwa kiasi cha mizigo iliyosafirishwa kwa Reli ya SGR nchini Kenya kimeongezeka kwa asilimia 24 hadi kufikia tani milioni 3.86 katika miezi tisa ya kwanza ya mwaka huu, ikilinganishwa na tani milioni 3.12 mwaka jana kipindi kama hicho, kutokana na biashara kuongezeka wakati uchumi wa nchi hiyo ukiendelea kufufuka.

Ripoti hiyo imesema kuongezeka huko pia kumeshuhudia ongezeko la mapato ya reli hiyo hadi karibu dola milioni 89 za kimarekani katika miezi 9 ya kwanza ya mwaka huu, ambapo idadi ya abiria waliotumia reli hiyo pia imeongezeka hadi kufikia milioni 1.37 katika kipindi hicho, ikilinganishwa na laki 4.2 ya mwaka jana.