Kampuni ya Huawei yatoa mafunzo kwa wanafunzi 50 wa Tehama nchini Malawi
2021-11-24 08:36:13| CRI

Kampuni ya teknolojia ya Habari na Teknolojia ya China Huawei imetoa mafunzo kwa wanafunzi 50 kutoka vyuo vikuu vya Malawi, chini ya programu yake iitwayo “Seeds for the Future”.

Mafunzo hayo yanayoitwa Mkutano wa Mageuzi ya Dijitali ya Kiviwanda, yaliyofanyika kuanzia Novemba 15 hadi Jumanne mjini Lilongwe, yametoa vyeti kwa vijana waliopata ujuzi mpya kuhusu Tehama.

Mwakilishi wa Huawei nchini Malawi Angela Chuma amesema, mafunzo ya mwaka huu yamewapa wanafunzi fursa ya kutambua thamani ya Tehama kupitia mawasiliano na wataalamu wa Tehama wa kampuni hiyo.

Bi. Chuma amesema kampuni yake inaamini kuwa ujuzi walioupata wanafunzi hao utatoa mchango mkubwa kwenye maendeleo ya nchi hiyo kwa kutumia Tehama.