Polisi wa Nigeria wamewaokoa watu 24 waliotekwa nyara katika eneo la kaskazini-magharibi
2021-11-24 11:05:23| CRI

Polisi wa Nigeria wamethibitisha kuwa watu 24 waliotekwa nyara wakiwemo wanafunzi watano wameachiwa uhuru wakati wa operesheni za uokoaji zilizofanywa hivi karibuni na polisi katika jimbo la Zamfara.

Mkuu wa polisi katika jimbo la Zamfara Bw. Ayuba Elkanah amesema mateka hao wote walikabidhiwa kwa serikali ya jimbo Jumanne. Aliongeza kuwa wanafunzi hao watano walitekwa nyara na watu wenye silaha wasiojulikana kutoka shule mbili huko Shinkafi na Kaura Namoda mwezi Septemba, na wameokolewa bila masharti.