China yapinga Marekani kumwalika kiongozi wa Taiwan kushiriki kwenye eti mkutano wa kilele wa demokrasia
2021-11-25 09:14:55| cri

China yapinga Marekani kumwalika kiongozi wa Taiwan kushiriki kwenye eti mkutano wa kilele wa demokrasia_fororder_台湾

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Bw. Zhao Lijian amesema China inapinga kithabiti Marekani kumwalika kiongozi wa Taiwan kushiriki kwenye eti mkutano wa kilele wa demokrasia.

Bw. Zhao amesema kuna China moja tu duniani, serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ni serikali pekee halali duniani inayoiwakilisha China, na Taiwan ni ardhi isiyotengeka ya China. China Moja ni kanuni iliyotambuliwa duniani katika mahusiano ya kimataifa, na Taiwan haina hadhi yoyote ya kisheria ya kimataifa licha ya kuwa sehemu ya China.

Ameikumbusha Marekani kufuata kithabiti sera ya kuwepo kwa China Moja, na taarifa tatu za pamoja za China na Marekani, na kusitisha kuwapa nafasi  watu wanaotaka kuitenga Taiwan kutoka China.

Akizungumzia eti mkutano wa kilele wa demokrasia utakaoandaliwa na Marekani, Bw. Zhao amesema demokrasia ni haki ya binadamu wote duniani, si haki ya kipekee ya nchi fulani. Kitendo cha Marekani kimeonyesha kuwa eti demokrasia yake ni nyenzo ya kupunguza ushawishi wa nchi zingine, kufarakanisha dunia na kulinda umwamba wake.