Rais Xi Jinping ataka kuharakishwa ujenzi wa mfumo wa kuhakikisha kujitegemea kwenye sayansi na teknolojia
2021-11-25 08:28:06| CR

Rais Xi Jinping wa China jana Jumatano aliongoza mkutano wa 22 wa kamati kuu ya kuimarisha mageuzi, ambao umejadili na kupitisha Mpango wa Miaka Mitatu wa Kuendeleza Teknolojia Muhimu Kwenye Mageuzi ya Kimfumo ya Sayansi na Teknolojia, na Mwongozo wa Kuharakisha Ujenzi wa Mfumo wa Taifa wa Soko la Pamoja la Umeme.

Rais Xi amesisitiza kuharakishwa ujenzi wa mfumo wa kuhakikisha kujitegemea kwenye sayansi na teknolojia za hali ya juu, na kuongeza uwezo wa kufanya mavumbuzi kimfumo katika tasnia ya sayansi na teknolojia. Pia ametaka kuboreshwa kwa usanifu wa jumla wa soko la umeme, na kuharakishwa ujenzi wa mfumo wa soko la pamoja la umeme ulio wazi, salama, wenye ufanisi na usimamizi kamili na kuruhusu ushindani wa haki.