Mkutano wa 5 wa Baraza la Viongozi Vijana kati ya China na Afrika wafanyika
2021-11-25 14:25:29| CRI

Mkutano wa 5 wa Baraza la Viongozi Vijana kati ya China na Afrika wafanyika_fororder_微信图片_20211125142213

Mkutano wa 5 wa Baraza la Viongozi Vijana kati ya China na Afrika na Mkutano wa kutoa Maelezo kuhusu Maudhui Makuu ya Mkutano wa 6 wa wajumbe wote Kamati Kuu ya 19 ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) umefunguliwa jana hapa Beijing.

Akihutubia mkutano huo, Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Nje ya Kamati Kuu ya CPC Bw. Song Tao ametoa ufafanuzi kuhusu maudhui makuu ya Mkutano wa 6 wa wajumbe wote Kamati Kuu ya 19 ya CPC, akisema vijana ni matumaini ya nchi na taifa, na ni mustakabali wa urafiki kati ya China na Afrika. Amesema daima CPC inazingatia na kuunga mkono masuala ya vijana wa China na Afrika, na pande hizo mbili zimetoa hatua mbalimbali za kuhimiza mawasiliano na ushirikiano kati ya vijana, na kuunga mkono vijana kuanzisha shughuli zao, ili kuongeza uwezo wa kujiendeleza kwa vijana wa Afrika.

Bw. Song Tao ametoa mapendekezo matatu kuhusu kuenzi urafiki kati ya China na Afrika na kujenga kwa pamoja enzi mpya ya ushirikiano kati ya China na Afrika. Amesema vijana wa China na Afrika wanapaswa kuwa washiriki wa mawasiliano kuhusu uzoefu wa utawala wa nchi, ili kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo na ustawishaji wa nchi mbalimbali, wanapaswa kupanua ushirikiano wa kirafiki kati ya pande hizo mbili na kutia nguvu katika kuenzi urafiki na kuzidisha uhusiano kati ya China na Afrika katika enzi mpya, na mwisho wanapaswa kuhimiza maendeleo ya ustaarabu wa binadamu, ili kutoa mchango wa vijana kwa ajili ya kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja ya binadamu.

Akizungumza kwenye mkutano huo, katibu mkuu wa chama cha Jubilee cha nchini Kenya, Raphael Tuju amesema, mfano wa China wa kujiendeleza kuwa nchi yenye nguvu ya kichumi umeleta matumaini kwa nchi za Afrika. Ameongeza kuwa vijana wa Afrika wanapaswa kuchunguza kwa kina mfumo wa kujiendeleza wa China, ili kupata ustawi wa Afrika.

Wajumbe vijana zaidi 200 kutoka vyama 52 vya siasa katika nchi 43 za Afrika wanahudhuria mkutano huo wa siku mbili.