DRC kuanzisha baraza la betri ili kuhimiza matumizi ya nishati safi
2021-11-25 09:12:33| CRI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC Jean-Michel Sama Lukonde jana jumatano alitangaza katika ufunguzi wa kongamano la biashara ya DRC-Afrika kwamba nchi hiyo itaanzisha baraza la betri ili kuhimiza maendeleo ya nishati safi.

Kongamano hilo la siku mbili lililoitishwa na serikali ya DRC lililenga kuhimiza uwekezaji ili kuiingiza Afrika kwenye mnyororo wa thamani wa sekta za betri, magari ya betri (EV) na nishati endelevu.

Rais Felix Tshisekedi wa nchi hiyo alisema DRC lazima ichukue nafasi ya kimkakati katika mchakato wa kuhimiza nishati safi.