Matukio ya wanawake na watoto kudhalilishwa kwa aina mbalimbali yanaonekana kushika kasi, na ingawa watu wanaofanya vitendo hivyo wanakemewa lakini inaonekana kama wadau wanampigia mbuzi gitaa, kwani wengi wao huendelea na vitendo hivyo. Udhalilishaji kwa wanawake na watoto uko wa aina nyingi tu, ukiwemo kubaka, kulawiti, kuingiliwa kinyume na maumbile, kutoroshwa, kuuliwa, kushambuliwa kwa aibu, kuvuliwa nguo au kushikwa maumbile yao ambapo baadhi ya watendaji wa vitendo hivi wanaachwa tu bila kuchukuliwa hatua zozote. Hivyo kwa kuzingatia machungu yanayomkabili mwanamke na mtoto leo tutazungumzia vitendo hivi ndani ya ukumbi wa wanawake.