Mkutano wa 8 wa mawaziri wa FOCAC kuimarisha zaidi ushirikiano wa kupambana na janga la COVID-19 kati ya China na Afrika
2021-11-26 16:24:13| CRI

Ofisa wa idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje ya China Balozi Zhao Baogang amesema, Mkutano wa 8 wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) utapitisha nyaraka nne za Azimio la Dakar, mpango wa utekelezaji, azimio la ushirikiano wa mabadiliko ya hali ya hewa kati ya China na Afrika, na mpango wa mwaka 2035 wa ushirikiano kati ya China na Afrika, ili kutoa mpango mzuri kwa ajili ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili katika miaka mitatu ijayo na miaka 15 ijayo.

Balozi Zhao amesema hayo alipohudhuria Baraza la Viongozi Vijana kati ya China na Afrika lililofanyika Beijing. Balozi Zhao amesema, China itaendelea kutoa hatua mpya za ushirikiano kati yake na Afrika, kufuatilia sekta zinazofuatiliwa zaidi na nchi za Afrika, zikiwemo ushirikiano wa kupambana na COVID-19, usalama wa chakula, maendeleo ya kilimo na mabadiliko ya hali ya hewa. Hatua hizo mpya zitaunga mkono Afrika kuondoa pengo la chanjo ya COVID-19 na kujenga ulinzi dhidi ya virusi vya Corona.

Mkutano wa 8 wa mawaziri wa FOCAC utafanyika tarehe 29 hadi 30 Novemba huko Dakar, mji mkuu wa Senegal.