Raphael Tuju: Vijana wa Afrika wapaswa kuchunguza mtindo wa maendeleo ya China, ili kuhimiza maendeleo barani Afrika
2021-11-26 14:16:16| CRI

Raphael Tuju: Vijana wa Afrika wapaswa kuchunguza mtindo wa maendeleo ya China, ili kuhimiza maendeleo barani Afrika_fororder_微信图片_20211126141545

Katibu mkuu wa chama tawala cha Kenya Jubilee Bw. Raphael Tuju amehudhuria Mkutano wa 5 wa Baraza la Viongozi wa Vijana kati ya China na Afrika na Mkutano wa Kufafanua Maudhui Makuu ya Mkutano wa 6 wa awamu ya 19 ya wajumbe wote wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC kwa njia ya mtandao.

Tuju amepongeza maadhimisho ya miaka 100 ya Chama cha Kikomunisti cha China, na kusema, chini ya uongozi wa CPC, China imepata maendeleo ya kasi ya uchumi, hali ambayo imeleta matumaini kwa nchi za Afrika. Katika mwaka 1973, jengo la juu zaidi nchini Kenya lilikuwa na ghorofa 28, wakati ule jengo la juu zaidi nchini China lilikuwa na ghorofa 26 tu, lakini sasa majengo 6 kati ya majengo 10 ya juu zaidi duniani yako nchini China. Aidha, mwaka 1978, thamani ya uzalishaji wa ndani ya Kenya GDP kwa kila mtu ilikuwa mara mbili ya China, lakini sasa China imekuwa nchi ya pili yenye uchumi kubwa duniani.

Ametoa wito kwa vijana wa Afrika kuchunguza kwa kina mtindo wa kujiendeleza wa China, kujua sababu ya China kupata maendeleo ya kasi ya uchumi katika muda mfupi, ili kutoa mchango katika maendeleo ya Afrika.

Bw. Tuju pia amesisitiza kuwa Kenya itaendelea kuunga mkono kanuni ya kuheshimiana na kutoingilia kati mambo ya ndani ya upande mwingine, kushikilia sera ya “kuwepo kwa China Moja”, kupinga kulichukua suala la haki za binadamu kuwa la kisiasa. Ameongeza kuwa, CPC inashikilia njia ya demokrasia yenye umaalumu wa China, hivyo nchi nyingine hazina haki ya kukilaumu.