AFDB kuiunga mkono Kenya kuhamasisha rasilimali fedha katika juhudi za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi
2021-11-26 09:01:29| cri

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AFDB) itaikia ombi la Kenya kwa kuiunga mkono katika kuhamasisha rasilimali fedha ili kuhimiza mpito wa uchumi wa kijani wakati nchi hiyo inakabiliwa na matukio ya hali mbaya ya hewa.

Makamu wa mkuu wa Benki ya AfDB anayeshughulikia mambo ya umeme, nishati, tabia nchi na ukuaji wa kijani Bw. Kevin Kariuki amesema benki hiyo itaendelea kufanya kazi ya uongozi katika uhamasishaji wa raslimali nchini humo kupitia ushirikiano wa kifedha wa Afrika katika mambo ya mabadiliko ya tabia nchi ulioanzishwa mwaka 2018.

Bw. Kariuki ameeleza kuwa benki hiyo itachangia uzoefu wake katika kukuza ustahimilivu wa jamii kupitia miradi kama vile mpango wa usambazaji maji katika miji midogo na vijijini. Alisema serikali katika kaunti zinatakiwa kufanya kazi muhimu kuhakikisha bajeti inatengwa ili kutekeleza hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.