Waraka mweupe wasema, China na Afrika zasimama pamoja katika masuala muhimu
2021-11-26 11:01:28| CRI

Waraka mweupe wasema, China na Afrika zasimama pamoja katika masuala muhimu_fororder_timg (2)

Waraka mweupe uliotolewa leo ijumaa na Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China unaoitwa “China na Afrika katika Zama Mpya: Uhusiano wa Usawa”, umesema China na Afrika daima zinasimama pamoja kithabiti katika maamuzi na masuala ya muhimu.

Waraka huo umesema, nchi za Afrika zimeunga mkono hatua za China za kulinda mamlaka yake, usalama na maendeleo, kuboresha muungano, na kutimiza ufufukaji wa taifa kupitia maendeleo.

China pia imeziunga mkono nchi za Afrika katika kutimiza uhuru wa kitaifa, kufuata njia za maendeleo zinazoendana na mazingira ya nchi husika, kuboresha maingiliano ya kikanda, na kuzisaidia nchi hizo kujiimarisha kupitia umoja.

Waraka huo umesema, mshikamano kati ya China na Afrika umewezesha pande hizo kukabiliana na matatizo na vikwazo, na kujenga siku nzuri za baadaye.

Kuhusu janga la COVID-19, waraka huo umesema pande hizo mbili zimevumilia majaribu makubwa, kusaidia na kupambana bega kwa bega kushinda janga hilo kupitia mshikamano na ushirikiano.