Rais wa China azungumzia uhusiano kati ya China na Afrika
2021-11-29 08:23:26| CRI

Rais Xi Jinping wa China atahudhuria ufunguzi wa mkutano wa ngazi ya mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) kwa njia ya mtandao.
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika huko Dakar nchini Senegal kuanzia Novemba 29 hadi 30 mwaka huu.

Mwezi Juni mwaka jana, Rais Xi Jinping wa China alitoa hotuba kwenye Mkutano wa Kilele wa Mshikamano na Ushirikiano katika kupambana na COVID-19, akisema,

Mlipuko wa ghafla wa COVID-19 umekuwa mzigo mkubwa kwa nchi mbalimbali duniani, huku malaki ya maisha ya thamani yakipotea. Hapa, ninapendekeza kuwa tuwe na muda wa kukaa kimya kuwakumbuka wale waliofariki kutokana na COVID-19, na kutoa rambirambi zetu kwa familia zao.

Katika hotuba yake, Rais Xi amependekeza kushirikiana kukabiliana na ugonjwa huo, kusukuma mbele ushirikiano kati ya China na Afrika, kutekeleza utaratibu wa pande nyingi, kuhimiza urafiki kati ya China na Afrika, na kujenga kwa pamoja jamii yenye hatma ya pamoja.
Kufanyika kwa mkutano huo si kama tu kumeonesha nia ya China ya kutimiza ahadi yake ya kuwa karibu zaidi na Afrika, bali pia kumeonesha imani na nia ya China ya kulinda utaratibu wa pande nyingi, na kuchangia ushirikiano wa kimataifa katika kukabiliana na virusi vya Corona.