Rais wa Afrika Kusini aonya kuwa nchi hiyo itakumbwa na wimbi la nne wakati virusi vya Omicron vikienea zaidi
2021-11-29 10:59:46| cri

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini jana alisema sasa virusi vipya vya Omicron vipo katika mikoa yote nchini humo, ikimaanisha kuwa Afrika Kusini inaweza kuingia kwenye wimbi la nne la janga kama idadi ya maambukizi mapya itaendelea kuongezeka.

Ramaphosa amesema utambuzi wa virusi vya Omicron unaendana na ongezeko la kasi la maambukizi ya COVID-19, ambapo idadi ya wastani ya maambukizi mapya imefikia 1,600 kwa siku katika siku 7 zilizopita. Kama idadi ya maambukizi itaendelea kuongezeka, nchi hiyo inakaridiwa kuwa na wimbi la nne la maambukizi ndani ya wiki kadhaa zijazo.