WHO yasema zuio la usafiri linatakiwa kuchukuliwa chini ya msingi wa sayansi
2021-11-29 11:00:15| cri

Ofisi ya Shirika la Afya Duniani (WHO) barani Afrika jana ilisema katika mapambano dhidi ya virusi vya Corona nchi zote zinapaswa kuchukua hatua za zuio la usafiri chini ya msingi wa sayansi na “Kanuni za afya za kimataifa (2005)”.

Ili kuzuia kuenea kwa virusi vipya vya Omicron, nchi nyingi zimechukua hatua za zuio la usafiri na kuimarisha hatua za udhibiti wa virusi dhidi ya ndege na wasafiri kutoka nchi za Afrika ikiwemo Afrika Kusini. Kwenye taarifa yake Ofisi hiyo imesema hatua za zuio la usafiri zinaweza kufanya kazi katika kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi vya Corona, lakini zitaziletea nchi mbalimbali shinikizo kubwa katika maisha yao, pia zitaharibu mshikamano wa dunia. Nchi zote zinapaswa kuchukua hatua za zuio chini ya msingi wa sayansi na “Kanuni za afya za kimataifa (2005)”.