Afrika na China kuendeleza zaidi lengo la ustawi wa pamoja
2021-11-30 08:38:53| CRI

Afrika na China kuendeleza zaidi lengo la ustawi wa pamoja_fororder_1128113735_16382045757441n

Rais wa Senegal, Macky Sall, amesema Afrika na China zinataka kuendeleza zaidi maslahi yao ya pamoja ili kutimiza ustawi wa pamoja kwa ajili ya watu wa pande hizo mbili.

Katika hotuba yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ulioanza jana mjini Dakar, Senegal, rais Sall amesema, tangu kuanzishwa kwa FOCAC miaka 21 iliyopita, Afrika na China zimeendelea kwa pamoja kwa ufanisi, kama inavyodhihirika kwa kuongezeka kwa biashara kati ya pande hizo mbili, uwekezaji, na mafanikio mengi chini ya mipango mingi. Pia ameishukuru China kwa kuendelea kuiunga mkono Afrika katika kufufua uchumi wake baada ya janga la virusi vya Corona.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Felix Tshisekedi ambaye ni Mwenyekiti wa sasa wa Umoja wa Afrika amesema, mkutano wa FOCAC, kupitia majadiliano ya kina na ya kiujenzi, utaangalia mafanikio yaliyofikiwa tangu kuanzishwa kwa Baraza hilo, na kutafuta mwelekeo mpya wa ushirikiano wa China na Afrika katika miaka mitatu ijayo.