Hotuba ya rais wa China katika mkutano wa FOCAC inaonyesha mwelekeo wa uhusiano wa China na Afrika
2021-12-01 08:45:57| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi amesema, hotuba iliyotolewa na rais wa China Xi Jinping katika mkutano wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) inatoa mwelekeo wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika.

Akizungumza na vyombo vya habari vya China mjini Dakar baada ya mkutano huo kumalizika, Wang Yi amesema, katika mkutano huo, rais Xi na viongozi wa Afrika walijadiliana kwa pamoja mpango wa maendeleo ya China na Afrika. Pia kutoa mwongozo wa maendeleo ya baadaye ya uhusiano kati ya pande hizo mbili ambao ni muhimu katika kuimarisha ushirikiano wa kimkakati na uhusiano kati ya China na Afrika, kuboresha mshikamano na ushirikiano kati ya nchi zinazoendelea, na ushirikiano wa kimataifa katika kupambana na janga la COVID-19, na kufanya mfumo wa utaratibu wa kimataifa na uongozi kuwa wa usawa zaidi.