China yasema, kinachodaiwa kuwa “Mkutano wa kilele wa Demokrasia” hautafaulu
2021-12-01 08:42:24| CRI

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian jana amesema, Marekani inaitisha kile kinachoitwa “Mkutano wa kilele wa Demokrasia”, na kuvunja demokrasia kwa kisingizio cha “kuhimiza demokrasia”, hatua ambayo ni kinyume na jumuiya ya kimataifa na haitafanikiwa.

Bw. Zhao Lijian amesema, Marekani inashikilia kulazimisha kile kinachoitwa “demokrasia” kwa nchi nyingine, na kuingilia kati mambo ya ndani ya nchi nyingine na kufanya uvamizi wa kijeshi, mambo yanayosababisha vurugu, vita na wakimbizi kwa nchi husika.

Ameongeza kuwa, kiini cha kile kinachoitwa “mkutano wa kilele wa demokrasia” ni kufufua wazo la vita baridi, kuchochea ufarakanishaji na upinzani, mambo ambayo hayakubaliki na hayatafanikiwa.