Katibu mkuu wa UM asema kupata chanjo kote duniani ni njia pekee ya kuzuia janga la Corona
2021-12-01 12:36:13| cri

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana alihutubia Mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa “Kundi la nchi 77 na China” akisema kupata chanjo kote duniani ni njia pekee ya kuzuia janga la Corona.

Amesema janga la Corona linaendelea kuziharibu vikali nchi zilizoendelea na zinazoendelea. Umoja wa Mataifa unaunga mkono mkakati wa kupata chanjo uliowekwa na Shirika la Afya Duniani (WHO), ambao lengo lake ni kuwapatia chanjo asilimia 40 ya watu wa nchi zote ndani ya mwaka huu, na kuwapatia chanjo asilimia 70 ya watu duniani hadi katikati ya mwaka 2022.