Pande zote za mazungumzo ya Vienna kuhusu makubaliano ya nyuklia ya Iran zakubali kuweka kipaumbele kuondoa vikwazo dhidi ya Iran
2021-12-01 09:06:58| cri

 

 

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ambaye pia ni Mwakilishi Mkuu wa Masuala ya Nyuklia ya Iran Ali Baqeri jana amesema, katika siku ya kwanza ya kuanza tena kwa mazungumzo ya makubaliano ya nyuklia ya Iran huko Vienna, pande husika zimekubali kutoa kipaumbele kwa suala la kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Iran katika mazungumzo hayo.

   Baqeri pia amesema washiriki wengi wanakubaliana na maoni ya Iran, kwamba ni muhimu kuhakikisha kuwa Marekani haitaiwekea vikwazo tena Iran na kwamba haitajiondoa katika makubaliano ya nyuklia ya Iran kama ilivyokuwa wakati wa utawala wa serikali iliyopita chini ya rais Donald Trump.