Mkutano wa 45 wa mawaziri wa mambo ya nje wa “Kundi la nchi 77 na China” wafanyika
2021-12-01 12:35:48| cri

Mkutano wa 45 wa mawaziri wa mambo ya nje wa “Kundi la nchi 77 na China” umefanyika jana kwa njia ya video.

Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Zhang Jun ameshiriki na kuhutubia mkutano huo. Kwenye hotuba yake, Zhang amesifu kazi ya uongozi ya Guinea ikiwa ni nchi mwenyekiti wa Kundi la nchi 77 katika mwaka 2021, na kuipongeza Pakistan kuwa nchi mwenyekiti wa kundi hilo kwa mwaka 2022.

Zhang amesema “Kundi la nchi 77 na China” zinapaswa kuimarisha mshikamano na kuweka mazingira mazuri katika kuharakisha ufufukaji wa nchi zinazoendelea baada ya janga la Corona na kutelekeza Ajenda ya mwaka 2030. China siku zote ni mwenzi wa kuaminika wa nchi zinazoendelea, itajitahidi kuhimiza Ushirikiano wa Kusini na Kusini na kuimarisha kuzijengea uwezo wa maendeleo nchi zinazoendelea.