Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema, marufuku kamili ya usafiri haitazuia kuenea kwa aina mpya ya virusi vya Omicron kimataifa, na itakuwa mzigo mkubwa kwa maisha ya watu.
Taarifa iliyotolewa na Shirika hilo imesema, jumapili iliyopita Shirika hilo liliorodhesha virusi hivyo kama virusi vinavyohitaji kufuatiliwa, na tangu wakati huo, nchi nyingi zimeweka vikwazo vya muda vya kusafiri, ikiwa ni pamoja na kupiga marufuku wasafiri kutoka nchi za kusini mwa Afrika, na kuzuia wasafiri kutoka nchi zilizogundulika kuwa na virusi hivyo.