Maambukizi mapya na vifo vya Ukimwi nchini Tanzania vyapungua
2021-12-02 08:37:41| CRI

 

 

Waziri mkuu wa Tanzania Bw. Kassim Majaliwa amesema maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi nchini Tanzania yamepungua kwa asilimia 38.2 kutoka laki 1.1 ya mwaka 2010 hadi elfu 68 ya mwaka 2020.

Katika hotuba yake ya kuadhimisha Siku ya kupambana na Ukimwi Duniani mkoani Mbeya, Bw. Majaliwa amesema vifo vinavyotokana na UKIMWI nchini Tanzania vimepungua kwa nusu kutoka vifo elfu 64 mwaka 2010 hadi vifo elfu 32 kwa mwaka 2020.

Bw. Majaliwa amesema mafanikio yaliyopatikana katika kupambana na Ukimwi yametokana na jitihada mbalimbali za ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na wadau wengine muhimu.