Rais wa Afrika Kusini alaani marufuku ya usafiri ya nchi za magharibi dhidi ya nchi yake kutokana na kugundua aina mpya ya virusi vya a COVID-19
2021-12-02 10:38:32| cri

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ambaye yuko ziarani nchini Nigeria amekosoa marufuku ya usafiri ya nchi za magharibi dhidi ya nchi za Afrika baada ya kugundua aina mpya ya virusi vya COVID-19.

Wakiongea na waandishi wa habari mjini Abuja na mwenyeji wake rais Muhammadu Buhari wa Nigeria, viongozi hao wameelezea kutoridhishwa na marufuku hiyo pamoja na viongozi wa Cote d'Ivoire, Ghana na Senegal. Rais Ramaphosa amesema janga la COVID-19 ni janga la kimataifa na linahitaji nchi zote zishirikiane na kufanya juhudi kwa pamoja ili kulishinda.