China na Afrika zaahidi kuimarisha ushirikiano katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi
2021-12-02 10:37:45| cri

China na Afrika zimetoa Azimio la ushirikiano juu ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, ambapo zimetambua kuwa mabadiliko ya tabianchi yamekuwa changamoto kubwa kwa mazingira ya ikolojia ya kimaumbile na maendeleo ya kijamii na kiuchumi ya China na Afrika.

Azimio hilo limesema pande zote mbili zimekubali juhudi na mchango mkubwa uliotolewa na China ikiwa ni nchi kubwa zaidi inayoendelea na bara la Afrika lenye nchi nyingi zaidi zinazoendelea juu ya kupunguza mabadiliko ya tabianchi. China na Afrika zimetambua kuwa mabadiliko ya tabianchi na shughuli za uhamiaji zinazosababishwa na suala hilo ni changamoto ya pamoja ya binadamu wote wanayokabiliana nayo. Zinahimiza nchi zote zifanye juhudi kwa pamoja chini ya mfumo wa pande nyingi.

Azimio hilo pia limesema nchi zilizoendelea zinapaswa kutekeleza wajibu wa kutoa fedha kwa ajili ya kuzisaidia nchi zinazoendelea hasa nchi za Afrika katika kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.