Mpango mpya wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika wakamilika
2021-12-02 08:24:51| CRI

Mpango mpya wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika wakamilika_fororder_汪文斌

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Wang Wenbin, amesema Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika umepata matokeo makubwa ambayo yameonyesha kiwango cha juu cha ushirikiano kati ya pande hizo mbili, na nia ya China na nchi za Afrika ya kutafuta maendeleo kwa pamoja, kukabiliana na changamoto kwa pamoja, na kunufaika na fursa kwa pamoja.

Bw. Wang amesema mpango mpya wa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika katika miaka mitatu ijayo na baadaye umekamilika, kuzingatia uaminifu na kutimiza ahadi ni umaalumu wa ushirikiano wa China na Afrika.

Amesema China itaendelea kushirikiana na nchi za Afrika, kuendelea kuenzi ushirikiano wa kirafiki kati ya pande hizo mbili, kuhimiza matokeo yaliyofikiwa kwenye mkutano huo kutelekezwa kwa hatua madhubuti, na kuanzisha hali mpya ya mandeleo ya ushirikiano huo yenye sifa ya juu, kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja kati ya China na Afrika katika zama mpya, ili kufanya juhudi na kutoa mchango kwa ajili ya kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakabali wa pamoja.