Rais Xi Jinping apongeza China kuadhimisha miaka 80 ya matangazo ya kimataifa
2021-12-03 20:41:51| cri

Rais wa China Xi Jinping leo ametoa salamu za pongezi kwa maadhimisho ya miaka 80 tangu China ianze huduma za matangazo ya kimataifa. Rais Xi ametoa salamu hizo kwa wafanyakazi wa Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, pamoja na marafiki wageni ambao wameunga mkono kazi za matangazo ya kimataifa za China.

Tarehe 3 Desemba 1941, Chama Cha Kikomunisti cha China kilianzisha kituo cha matangazo ya Radio mjini Yan'an kikitangaza kwa lugha ya Kijapan, na kuwa mwanzo wa matangazo ya kimataifa ya China.